28 Juni 2026 - 11:29
IRGC Yatangaza Mashambulizi Makali zaidi ya Makombora na Ndege zisizo na Rubani Kujibu Uchokozi wa Marekani

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuanzisha operesheni za makombora na ndege zisizo na rubani kujibu kile lilichokiita uchokozi wa Marekani, huku likionya kuwa litachukua hatua kali zaidi dhidi ya meli zitakazokiuka maelekezo yake.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limejibu chokochoko za Kijeshi za Marekani kwa kuzishambulia kwa Droni na Makombora Kambi za Kijeshi za Marekani zilipo Kuwait na Bahrain na kutangaza rasmi kuwa kuanzia sasa operesheni za kimkakati za kutumia makombora na ndege zisizo na rubani (droni) kujibu mashambulizi na uchokozi wa Marekani dhidi ya Iran zitaendelea kwa nguvu kubwa zaidi ya mashambulizi yake ya Leo Jumapili asubuhi.

Katika taarifa yake, IRGC ilisema kuwa hatua hizo ni sehemu ya haki ya kujilinda na kulinda usalama wa taifa la Iran dhidi ya vitendo vya uhasama vya Marekani. 

Aidha, jeshi hilo limeonya kwamba kuanzia sasa litachukua hatua kali zaidi dhidi ya meli zozote zitakazokiuka maelekezo na tahadhari zilizotolewa katika maeneo ya operesheni.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha